Maisha yangu: Miaka minane ndani ya Baraza la Mapinduzi: Khaini au mhanga wa mapinduzi ?

Maisha yangu: Miaka minane ndani ya Baraza la Mapinduzi: Khaini au mhanga wa mapinduzi ?

Paperback (25 Mar 2022) | Swahili

Not available for sale

Includes delivery to the United States

Out of stock

This service is protected by reCAPTCHA and the Google Privacy Policy and Terms of Service apply.

Publisher's Synopsis

"MAISHA YANGU: KHAINI AU MUHANGA WA MAPINDUZI YA ZANZIBAR?" ni kitabu kinachoeleza historia ya Zanzibar ya hivi karibuni na vipi Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika ulivyoanzishwa hadi kuwepo taifa jipya la TANZANIA. Khamis Abdulla Ameir amejaribu kwa kadri ya uwezo wake kuweka sawa historia ya Muungano wa Tanzania katika njia iliokuwa sahihi kabisa, ili Watanzania wa leo na wa vizazi vijavyo, waweze kuelewa chanzo na malengo halisi ya Muungano huu. Kitabu hiki kinasimulia historia mpya ya kileo kuhusu vipi vyama vya siasa vilivyoanzishwa Zanzibar tokea mwanzoni mwa miaka ya 1950 na vipi vyama hivyo na vyama vya wafanyakazi vilivyodai uhuru wa Zanzibar kutoka kwa Balozi Mkaazi wa Uingereza na sio kutoka kwa Mfalme Mwarabu ambaye alikuwa hana sauti mbele ya Balozi wa Uingereza. Zanzibar ilipata uhuru wake tarehe 10 Disemba, 1963 na serikali ya mseto ya ZNP/ZPPP ikakabidhiwa madaraka baada ya kushinda katika uchaguzi. Mwandishi anaeleza vipi Mapinduzi ya Zanzibar yalivyotekwa nyara na Mabeberu wa Uingereza na Marekani kwa kushirikiana na Viongozi wakuu wa Kenya, Uganda na Tanganyika ili Zanzibar isiweze kutekeleza siasa ya Kisoshalisti, ambayo nchi hiyo ilishaanza kuitekeleza kivitendo. Frank Carlucci, jasusi maarufu wa CIA, alipelekwa Zazibar na serikali yake kwa kazi moja tu, nayo ni kuizuia Zanzibar isijekuwa CUBA YA AFRIKA na kuziambukiza siasa ya Usoshalisti nchi jirani za Afrika Mashariki na Afrika kwa jumla. Kitabu kilichapishwa na DL2A Buluu Publishing, jijini Paris, Ufaransa.

Book information

ISBN: 9791092789232
Publisher: Lulu Press
Imprint: Diffusion Des Litteratures En Langues Africaines
Pub date:
Language: Swahili
Number of pages: 588
Weight: 948g
Height: 210mm
Width: 148mm
Spine width: 41mm