Publisher's Synopsis
Udhibiti ni njia mojawapo inayotumika kusimamia Uchumi wa nchi na kuendeleza ustawi wa jamii.Udhibiti wa huduma za kiuchumi (public utilities) unahusu kuweka mizania kati ya kuwawezesha watoa huduma na kuwalinda watumiaji wa huduma kama vile maji, umeme, uchukuzi, mawasiliano na utangazaji. Kitabu hiki kinaelezea chimbuko la udhibiti Tanzania katika muktadha wa mabadiliko ya uchumi duniani pamoja na udhibiti katika nchi nyingine.Ni kitabu chenye maarifa ya msingi kwa kila mtumiaji wa huduma za kiuchumi, pamoja na wanafunzi, wasomi, wafanyakazi na viongozi.